WAZIRI UMMY AMETOA MAONO YAKE JUU YA MNMH KUWA KITUO CHA UMAHIRI KWENYE MASWALA YA AFYA YA AKILI NA MAGONJWA YA AKILI
Waziri wa Afya Mhe. @ummymwalimu ameitaka Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe kujikita katika masuala ya kukuza Afya ya akili ikiwa ndiyo lengo mahususi la kuanzishwa kwa MNMH Akizungumza Mhe. Ummy amesema MNMH kuhusisha huduma za tiba ya Afya ya Akili, tafiti mbalimbali za maradhi hayo, mafunzo ya Afya za akili na kuhamasisha jamii kuwa na uelewa juu ya Afya ya akili.